غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يُجَـٰدِلُونَ فِىٓ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ بِغَيْرِ سُلْطَـٰنٍ أَتَىٰهُمْ ۖ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلْبِ مُتَكَبِّرٍ جَبَّارٍ ٣٥
{35} Kisha akataja maelezo ya mwongo huyo mwingi kupitiliza kiasi, akasema: "Hao ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu" ambazo zilibainisha haki mbali na batili, na zikawa kama jua kwa macho katika kubainika kwake. Wanabishana juu yake licha ya ubainifu wake, ili wazipinge na wazibatilishe "pasipo ushahidi wowote uliowafikia." Hii ndiyo sifa isiyoachana na kila anayepinga ishara za Mwenyezi Mungu. Haiwezekani kwake kubishana akitumia ushahidi, kwa sababu haki haiwezi kupingwa na mpinzani yeyote; kwa hivyo haiwezi kupingwa kwa ushahidi wa kisheria au wa kiakili hata kidogo. "Ni chukizo kubwa" kauli hiyo inayojumuisha kupinga haki kwa batili "mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wale walioamini." Mwenyezi Mungu ana chuki kubwa zaidi kwa afanyae hivyo, kwa sababu inajumuisha kuikadhibisha haki na kuisadiki batili na kumnasibisha nayo. Hayo yote ni mambo ambayo Mwenyezi Mungu huyachukia zaidi, na anamchukia yule anayesifika nayo, na pia waja wake waumini wanayachukia sana kwa kuafikiana na Mola wao Mlezi. Hawa ndio viumbe maalumu ambao Mwenyezi Mungu aliwaumba. Chuki yao ni ushahidi wa ubaya mkubwa wa wale ambao wao wanawachukia. "Hivi" alivyoziba nyoyo za familia ya Firauni, "ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kila moyo wa jeuri anayejivuna." Mwenye kiburi cha kukataa haki na cha kuwadharau viumbe wake, na anayejivuna kwa kufanya dhuluma nyingi na kuvuka kwake mipaka.