انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٦

وَقَالَ فِرْعَوْنُ ذَرُونِىٓ أَقْتُلْ مُوسَىٰ وَلْيَدْعُ رَبَّهُۥٓ ۖ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمْ أَوْ أَن يُظْهِرَ فِى ٱلْأَرْضِ ٱلْفَسَادَ ٢٦

{26} Na "Firauni akasema" kwa kiburi, kutakabari na kuwahadaa watu wake wapumbavu: "Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake Mlezi!" Yaani, alidai - Mwenyezi Mungu amlaani - kwamba kama haingekuwa ni kwa sababu ya kuzingatia hisia za watu wake, basi angemuua Musa na kwamba hata Musa akimuomba dua Mola wake Mlezi, hilo haliwezi kumzuia kufanya hivyo. Kisha akataja kile kilichomfanya kutaka kumuua Musa, na kwamba alikuwa anawapa watu wake nasaha ya sawasawa na kuwaondolea maovu katika ardhi. Akasema: "Mimi nachelea aje kukubadilishieni dini yenu" mnayoifuata, "au akadhihirisha uharibifu katika nchi." Hili ndilo jambo la kushangaza zaidi! Kwamba kiumbe muovu zaidi awe ndiye anayewashauri watu kutomfuata kiumbe bora zaidi. Huku ni kubadilisha mambo ambako hakuingii isipokuwa katika akili za wale ambao Mwenyezi Mungu alisema juu yao: "Basi aliwachezea watu wake, na wakamtii. Kwa hakika hao walikuwa watu wavukao mipaka."