انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٥

فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلْحَقِّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا۟ ٱقْتُلُوٓا۟ أَبْنَآءَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ وَٱسْتَحْيُوا۟ نِسَآءَهُمْ ۚ وَمَا كَيْدُ ٱلْكَـٰفِرِينَ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ ٢٥

{25} "Basi alipowaletea Haki inayotoka kwetu" na Mwenyezi Mungu akamsaidia kwa miujiza ya kung'aa iliyohitaji kusalimu amri kikamilifu, hawakuikabili kwa njia hiyo, na tena haikuwatosha kuiacha tu na kuipa mgongo, wala kuikataa na kuipinga kwa batili, bali hali yao mbaya hiyo iliwafikisha kiwango cha: "Waueni watoto wanaume wa wale waliomuamini na wawacheni hai wanawake wao. Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu." Kwa kuwa walipanga vitimbi hivi na wakadai kwamba wakiwauwa watoto wao wanaume, basi hawatakuwa na nguvu, na wataendelea kuwa katika utumwa chini ya umiliki wao. Lakini vitimbi vyao hivyo havikuwa "ila katika upotovu," kwani hayakutimia yale waliyokusudia, bali kiliwapata kinyume cha walichokusudia. Mwenyezi Mungu aliwaangamiza na kuwafutilia mbali hadi wa mwisho wao. Kanuni: Zingatia suala hili ambalo limetajwa mara kwa mara katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ikiwa muktadha unahusu hadithi maalumu au juu ya jambo maalumu, na Mwenyezi Mungu akataka kuhukumu jambo hilo maalum kwa hukumu ambayo sio mahususi kwa hilo tu. Yeye hutaja hukumu hiyo na akaifungamanisha na maelezo ya jumla; ili iwe ni hukumu ya jumla zaidi na ijumuishe suala hilo ambalo mazungumzo hayo yalikuja kwa sababu yake, ili kuzuia hisia kwamba hukumu hii ni maalumu kwa jambo hilo maalumu. Ndiyo maana hakusema: 'Na haviwi vitimbi vyao ila katika upotovu', bali alisema: "Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu."