انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤١

فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍۭ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰٓؤُلَآءِ شَهِيدًا ٤١

{41} Kisha Yeye Mtukufu akasema, “Basi itakuwa vipi tutakapoleta kutoka kwa kila umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi dhidi ya hawa?” Yani zitakuwaje hali hizo? Na itakuaje hukumu hiyo kubwa ambayo inakusanya kwamba anayehukumu kwayo ni Mwenye elimu kamili, Mwenye uadilifu kamili, Mwenye hekima kamili kwa ushahidi wa aliye safi zaidi wa viumbe, ambao ni Mitume, juu ya umma wao, pamoja na kukiri kwa yule aliyehukumiwa? Basi hii, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu ndiyo hukumu ambayo ndiyo ya jumla zaidi katika hukumu zote, na ya uadilifu yake zaidi, na kubwa yake zaidi. Na hapo anabaki yule aliyehukumiwa amemkiria ukamilifu wa fadhila, na uadilifu, na himdi, na sifa. Na hapo kaumu moja watafurahia kufuzu, na kufaulu, na utukufu, na kupita. Nao kaumu wengine watataabika kwa hizaya, na fedheha, na adhabu ya kudunisha.