النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَـٰعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا ٤٠
{40} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ukamilifu wa uadilifu wake na fadhila yake, na kutukuka kwake kutokana na yale yanayopingana na hayo miongoni mwa dhuluma chache na nyingi. Akasema, “Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja.” Yani haupunguzi (uzito huo) kutoka kwa matendo ya mja wake au kuuzidishia katika maovu yake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Basi anayetenda chembe ya wema, atauona! Na anayetenda chembe ya uovu atauona!” Na akasema, “Na ikiwa ni zuri, atalizidisha” Yani hadi mara kumi mfano wake, hadi zaidi ya hivyo kulingana na hali yake, na manufaa yake, na hali ya mwenyewe, na kumfanyia Yeye peke yake, na upendo, na ukamilifu. “Na atapeana kutoka kwake malipo makubwa.” Yani nyongeza juu ya thawabu za matendo yenyewe kama vile kuwawezesha kutenda matendo ya heri, na kutoa katika njia za wema kwa wingi, na kufanya heri tele.