انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١٦٨–١٦٩

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَظَلَمُوا۟ لَمْ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا ١٦٨ إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرًا ١٦٩

{168 - 169} Ndiyo maana akasema, "Hakika, wale waliokufuru na wakadhulumu." Na dhuluma hii ni ziada juu ya ukafiri wao, vinginevyo, wakati dhuluma inatajwa bila ya kufungiwa, basi ukafiri unaingia ndani yake. Na kilichomaanishwa na dhuluma hapa ni matendo ya ukafiri na kuzama ndani yake. Basi hawa wako mbali na kufutiwa dhambi, na kuongolewa kwenye njia iliyonyooka. Na ndiyo maana akasema, “Hakuwa Mwenyezi Mungu ni wa kuwafutia dhambi wala kuwaongoa njia. Isipokuwa njia ya Jahannamu.” Na kufutiwa dhambi kwao na kuongolewa hakukuwezekana kwa sababu waliendelea na uasi wao na wakazidi katika ukafiri wao, kwa hivyo nyoyo zao zikapigwa muhuri na zikawafungikia njia za uwongofu kwa sababu ya yale waliyoyachuma, na Mola wako si mwenye kuwadhulumu waja wake. "Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi." Yaani, Mwenyezi Mungu hawajali kwa sababu hawaifailii heri, wala haiendani nao isipokuwa hali waliyojichagulia wenyewe.