انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٧٠

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَـَٔامِنُوا۟ خَيْرًا لَّكُمْ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا۟ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ١٧٠

{170} Yeye Mtukufu anawaamrisha watu wote kwamba wamwamini mja wake na Mtume wake Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake, - na akataja sababu yenye kufanya kumwamini na faida ya kumwamini, na madhara ya kutoamini. Sababu yenye kufanya ni kujulisha kwake kwamba aliwajia kwa haki. Yani, Kuja kwake ni kwenyewe ni haki, na aliyokuja nayo miongoni mwa Sheria ni haki. basi mwenye akili timamu anajua kwamba watu kubaki katika ujinga wao wakitangatanga ovyo katika ukafiri wao na wakisitasita katika utume yalikwishawakatika, na hayafailii hekima ya Mwenyezi Mungu na rehema zake. Basi katika hekima yake na rehema Yake kuu ni huko kutuma kwenywe kwa Mtume kwao ili awajulishe uwongofu kutokana na upotofu, na makosa kutokana na usahihi. Basi kwa Kuangalia tu katika utume wake ni ushahidi wa uhakika juu ya usahihi wa unabii wake, na vile vile kuangalia katika kile alichokuja nacho miongoni mwa sheria tukufu, na njia iliyonyooka. Kwani ina habari za ghaibu zilizopita na zijazo, na habari juu ya Mwenyezi Mungu na juu ya Siku ya Mwisho ambazo haziwezi kuzijua isipokuwa kwa wahyi na utume, na yaliyo ndani yake miongoni mwa maamrisho kuhusu kila heri, na kutengenea, na uwongofu, na uadilifu, na ihsani, na ukweli, na wema , na kuunga uhusiano, na tabia njema. Na miongoni mwa kukataza maovu, uharibifu, na kupita mipaka, na dhuluma, na tabia mbaya, na uwongo, na kuwaasi wazazi, ambayo kwayo mtu anakuwa na uhakika kwamba yanatoka kwa Mwenyezi Mungu. Na kila mja anavyozidi ufahamu kupitia hayo, ndivyo kila inavyozidi Imani yake na yakini yake. Basi hii ndiyo sababu inayomwita mja kwenye imani. Na Ama manufaa katika kuamini, basi alijulisha kuwa hilo ni heri "kwenu." Nayo heri ni kinyume cha uovu. Basi Imani ni bora kwa Waumini katika miili yao, na nyoyo zao, na roho zao, na dunia yao na akhera yao. Na hilo ni kwa sababu ya yale yanayoambatana nayo miongoni mwa masilahi na faida. Kwa hivyo, kila thawabu ya sasa na ya baadaye ni katika matunda ya imani. Kwa hivyo, nusura na wongofu, na elimu na matendo mema, na furaha, na Pepo na yale yaliyo miongoni mwa neema, hayo yote ni kwa sababu ya imani. Kama vile taabu ya kidunia, na ya kiakhera ni kutokana na kutoamini au upungufu wake. Na Ama madhara ya kutomwamini yeye – Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani; - basi hayo yanajulikana kuwa kinyume cha matokeo ya kumwamini Yeye na kwamba, mja hamdhuru yeyote isipokuwa nafsi yake mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, na uasi wa muasi haumdhuru. Ndio maana akasema, "Hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo mbinguni na katika ardhi." Yaani, kila mtu ni kiumbe chake, mali yake, na chini ya usimamizi na udhibiti wake. "Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu," "Mwenye hekima" katika uumbaji wake na amri zake. Yeye ndiye Mjuzi wa nani anayestahiki uwongofu na majaribio, Mwenye hekima katika kuweka uwongofu na majaribu pahali pake panapostahiki.