انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الزمر
السورة ٣٩

الزمر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٥

وَتَرَى ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ حَآفِّينَ مِنْ حَوْلِ ٱلْعَرْشِ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ ۖ وَقُضِىَ بَيْنَهُم بِٱلْحَقِّ وَقِيلَ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ٧٥

{75} "Na utawaona Malaika" ewe mwenye kuona, siku hiyo kuu "wakizunguka pembeni mwa Kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu" wakimtumikia Mola wao Mlezi huku wamenyenyekea kwa sababu ya utukufu wake, wakikiri ukamilifu wake, "wakimtakasa na kumsifu Mola wao Mlezi" kutokana na yote yasiyoufailia utukufu wake, miongoni mwa yale ambayo washirikina walimnasibisha nayo na yale ambayo hawakumnasibisha nayo. "Na patahukumiwa baina yao" yaani, baina ya viumbe wa mwanzo na wa mwisho "kwa haki" isiyo na shaka yoyote wala hataweza kuikataa yule anayelazimika kuilipa, "Na patasemwa: Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote!" Hapa haikusemwa ni nani aliyeyasema hayo, ili hilo liashirie kwamba viumbe vyote vitazungumza kwa kumhimidi Mola wao Mlezi na hekima yake kwa yale aliyowahukumia watu wa Peponi na watu wa Motoni, na himdi ya fadhila zake na ukarimu wake, na himdi ya uadilifu wake na hekima yake.

Imekamilika tafsiri ya Surat Az-Zumar kwa sifa na msaada wa Mwenyezi Mungu.