انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الزمر
السورة ٣٩

الزمر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٩

فَإِذَا مَسَّ ٱلْإِنسَـٰنَ ضُرٌّ دَعَانَا ثُمَّ إِذَا خَوَّلْنَـٰهُ نِعْمَةً مِّنَّا قَالَ إِنَّمَآ أُوتِيتُهُۥ عَلَىٰ عِلْمٍۭ ۚ بَلْ هِىَ فِتْنَةٌ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ٤٩

{49} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu hali na maumbile ya asili ya mwanadamu kwamba yanapompata madhara, kama vile maradhi, ugumu au dhiki, "hutuomba" akikakamia tumpe afueni kutokana na yale yaliyompata. "Kisha tunapompa neema zitokazo kwetu" kwa kumwondolea madhara na ugumu wake, akarejea kwa Mola wake Mlezi akiwa ni kafiri na akakanusha neema yake, na "husema: Nimepewa haya kwa sababu ya elimu" ya Mwenyezi Mungu kwamba mimi ninaistahiki kwa sababu mimi ni mtukufu kwake. Au kwa sababu ya elimu ninayo ya kuichuma. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Sivyo! Huo ni mtihani" ambao Mwenyezi Mungu huwajaribu kwao waja wake ili aone ni nani atakayemshukuru na ni nani atakayemkufuru. "Lakini wengi wao hawajui!" Ndiyo maana wanachukulia kuwa mitihani hiyo zawadi, na hawaitofautishi heri tupu mbali na kitu kinachoweza kuwa sababu ya heri au uovu.