انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الصافات
السورة ٣٧

الصافات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤٩

فَٱسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ ٱلْبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلْبَنُونَ ١٤٩

{149} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Basi waulize" wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, waliowaabudu Malaika na wakadai kwamba hao ni mabinti za Mwenyezi Mungu, wakawa wamejumuisha kati ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa yasiyoufailia utukufu wake. "Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?" Huo ni mgawanyo wa dhuluma, kwa kumnasibishia Mwenyezi Mungu mwana, na pia kumfanyia mwana huyo kutoka kwa kiumbe wanachokiona duni zaidi, yaani mwana wa kike, ambaye hata wao wenyewe hawamridhii, kama alivyosema katika Aya nyingine: "Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu (Ametakasika)! Na wao wenyewe ati ndio wawe na hayo wanayoyatamani!" Na dhuluma yao kwa upande mwingine kwamba waliwafanya Malaika kuwa binti za Mwenyezi Mungu.