الصافات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَرْسَلْنَـٰهُ إِلَىٰ مِا۟ئَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ ١٤٧ فَـَٔامَنُوا۟ فَمَتَّعْنَـٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍ ١٤٨
{147 - 148} Kisha akamfanyia upole mwingine, na akampa neema kubwa ambayo ni kwamba alimtuma "kwa watu laki moja au zaidi." Kwa hivyo, akawalingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na "wakaamini," naye akalipwa kwa sababu ya hilo kwa kuwa yeye ndiye aliyewalingania. "Na tukawastarehesha kwa muda." Hilo lilikuwa kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwaondolea adhabu baada ya sababu zake kutokuwepo. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwa nini usiwepo mji mmoja ukaamini na Imani yake ikawafaa - isipokuwa kaumu ya Yunus? Waliamini na Sisi tukawaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia, na tukawastarehesha kwa muda."