فاطر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ ٧
{7} Kisha akataja kuwa watu wamegawanyika makundi mawili kulingana na kumtii kwao Shetani na kutomtii, na akataja malipo ya kila moja ya makundi hayo. Akasema: "Wale waliokufuru" yale waliyoyaleta Mitume na yakaashiriwa na Vitabu "watakuwa na adhabu kali" katika Moto wa Jahannamu, ambao huo wenyewe ni mkali sana na pia ni wenye sifa kali sana, na kwamba watakaa humo milele. "Na wale walioamini " kwa nyoyo zao yale aliyoyalingania Mwenyezi Mungu kwamba wayaamini, "na wakatenda mema" kwa mujibu wa imani hiyo kwa viungo vyao "watapata msamaha" kwa dhambi zao, na kwa hilo wataepushwa na shari na mambo wanayochukia "na" watapata "ujira mkubwa" ambao utawafanya kupata wanachokitaka.