النمل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَمَّن يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ قُلْ هَاتُوا۟ بُرْهَـٰنَكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ ٦٤
{64} Yaani, ni nani anayeanzisha uumbaji wa viumbe, na kisha ataurudia uumbaji huo siku ya ufufuo na kutawanyika? "Na ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi" kwa mvua na mimea? "Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu," anayefanya hivi na ana uwezo wa kufanya hivyo? "Sema: Leteni hoja zenu" na ushahidi wenu kwa kile mlichosema "kama nyinyi ni wakweli." Vinginevyo, kwa kuchukulia tu kwamba mnasema kuwa: Masanamu wanashirikiana naye katika baadhi ya hayo; basi hayo ni madai tu, kwa hivyo yathibitisheni kwa hoja, vinginevyo, jueni kuwa nyinyi ni wana batili, msiokuwa na hoja yoyote, kwa hivyo rudini kwenye ushahidi wenye yakini na hoja za kukata juu ya kwamba Mwenyezi Mungu ni wa kipekee katika matendo yote, na kwamba anastahiki kufanyiwa kila aina ya ibada.