النمل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَوْا۟ عَلَىٰ وَادِ ٱلنَّمْلِ قَالَتْ نَمْلَةٌ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّمْلُ ٱدْخُلُوا۟ مَسَـٰكِنَكُمْ لَا يَحْطِمَنَّكُمْ سُلَيْمَـٰنُ وَجُنُودُهُۥ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ١٨
{18} Na siku moja alisafiri na askari hawa wakubwa katika baadhi ya safari zake, "Mpaka walipofika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja" akiwatanabahisha wenzake na jamii yake: "Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asiwapondeni Suleiman na majeshi yake bila ya wao kutambua." Kwa hivyo mchwa huyu akawa amewanasihi na kuwaskizisha mchwa wenzake: ima yeye mwenyewe. Na ikiwa ni hivyo, inakuwa kwamba Mwenyezi Mungu aliwapa mchwa uwezo usio wa kawaida wa kusikia. Kwa sababu tanabahisho la mchwa huyo ambalo lililijaza bonde kwa sauti ya mchwa mmoja tu ni katika maajabu makubwa zaidi. Na ima aliwaambia mchwa waliomzunguka, kisha habari hiyo ikaenea kati yao kutoka kwa wenyewe hadi ikawafikia wote, na akawaamrisha kujitahadharisha na pia akawaambia njia ya kufanya hivyo, ambayo ni kuingia ndani ya makazi yao, na alijua hali ya Suleiman na askari wake na ukubwa wa mamlaka yake, na pia akampa udhuru kwa niaba yao ikiwa atawaangamiza, kwani hilo huenda likatokea si kwa kukusudia kwao wala kulihisi.