النمل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَحُشِرَ لِسُلَيْمَـٰنَ جُنُودُهُۥ مِنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ وَٱلطَّيْرِ فَهُمْ يُوزَعُونَ ١٧
{17} "Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu." Yaani, alipewa askari wake wengi mno wa aina mbalimbali miongoni mwa wanadamu, majini, mashetani na ndege; "nayo yakapangwa kwa nidhamu." Wakawa wanaendeshwa na kurudishwa wa kwanza wao kwa wa mwisho wao, na wakapangwa kwa nidhamu nzuri zaidi katika safari yao, kushuka kwao. Alikuwa amejiandaa vyema kwa ajili ya hili, na wakawa majeshi hawa wote wanatekeleza amri yake, na hawakuweza kumuasi na kumpinga. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu mtukufu, "Hiki ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hesabu."