الفرقان
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيْفَ مَدَّ ٱلظِّلَّ وَلَوْ شَآءَ لَجَعَلَهُۥ سَاكِنًا ثُمَّ جَعَلْنَا ٱلشَّمْسَ عَلَيْهِ دَلِيلًا ٤٥ ثُمَّ قَبَضْنَـٰهُ إِلَيْنَا قَبْضًا يَسِيرًا ٤٦
{45 - 46} Yaani, hukushuhudia kwa macho yako na ufahamu wako ukamilifu wa uwezo za Mola wako Mlezi na upana wa rehema zake: kwamba aliwatandazia waja kivuli. Na hilo ni kabla ya jua kuchomoza. "Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake." Kwa sababu, ikiwa jua halingekuwepo, basi kivuli kisingejulikana. Kwa maana, kitu hujulikana kwa kinyume chake. "Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo;" kwa kuwa, kila jua linapoinuka juu, kivuli kinapungua kidogo kidogo, mpaka kiondoke kabisa. Kwa hivyo, kufuatana kwa kivuli na jua ambako viumbe wanaona kwa macho yao, na yanayotokana na hilo kama vile kuwepo usiku na mchana na kubadilishana kwake, na misimu na kupatikana masilahi mengi kwa sababu yake, hayo yote ni katika ushahidi wenye kuonyesha zaidi uwezo na ukuu wa Mwenyezi Mungu, na ukamilifu wa rehema yake na utunzaji wake kwa waja wake, na kwamba Yeye peke yake ndiye muabudiwa, Msifiwa, Mpendwa, apewaye taadhima, Mwenye utukufu na ukarimu.