النور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُزْجِى سَحَابًا ثُمَّ يُؤَلِّفُ بَيْنَهُۥ ثُمَّ يَجْعَلُهُۥ رُكَامًا فَتَرَى ٱلْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَـٰلِهِۦ وَيُنَزِّلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن جِبَالٍ فِيهَا مِنۢ بَرَدٍ فَيُصِيبُ بِهِۦ مَن يَشَآءُ وَيَصْرِفُهُۥ عَن مَّن يَشَآءُ ۖ يَكَادُ سَنَا بَرْقِهِۦ يَذْهَبُ بِٱلْأَبْصَـٰرِ ٤٣
{43} Yaani hukuona kwa macho yako ukubwa wa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jinsi, "Anayasukuma;'' yaani, anaendesha ''mawingu:'' vipande vipande, ''kisha huyaambatisha,'' baina ya hizo, vipande vipande, na kuyafanya kuwa mawingu kama milima. ''Basi utaona mvua ikitoka kati yake;'' yaani, manyunyu na mvua zinazotoka katika mawingu kwa matone tofauti; ili manufaa hayo yapatikane bila madhara. Kwa hivyo mito itajazwa, mashimo yatapita, mabonde yatapita, na ardhi itakua kutoka kwa kila jozi ya ukarimu. Na wakati fulani Mwenyezi Mungu huteremsha mvua ya mawe kutoka kwenye wingu hilo na ikaharibu kila inachokipiga, ''akamsibu nayo amtakaye na akamuepusha nayo amtakaye.'' Yaani, kwa matakwa ya hukumu na hekima yake aliyosifiwa juu yake. ''Hukurubia mmetuko wa umeme wake,'' yaani, yakurubia mmetuko wa umeme wa hayo mawingu kutokamana na ukali wake; ''kupofua macho.'' Je, si yule aliyeiumba na akaielekeza kwa waja wake wenye haja na akaiteremsha kwa njia ya kuleta manufaa na kuepuka madhara, iliyojaa nguvu, yenye ufanisi katika mapenzi, na yenye rehema?