البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالُوا۟ سُبْحَـٰنَكَ لَا عِلْمَ لَنَآ إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَآ ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْحَكِيمُ ٣٢
(32) “Wakasema: Subhanaka (Wewe umetakasika!)” Yani: Tunakutakasa kutokana na pingamizi kutoka kwetu dhidi yako, na kuhalifu amri yako. “Hatuna elimu (ujuzi)” kwa njia yoyote ile “isipokuwa kwa uliyotufunza Wewe” kutokana na fadhila na ukarimu wako. “Hakika Wewe ndiye Mwenye elimu (Mjuzi), Mwenye hekima.” Al-‘Alim (Mwenye elimu) ni yule anayejua kila kitu, na kitu chochote hakikosekani kuwepo kwake. Na wala hakuna kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe, sio katika mbingu wala ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi. Al-Hakim (Mwenye hekima) ni yule mwenye hekima kamili ambayo hakuna kiumbe anayeweza kutoka ndani yake. Na wala hakuna aliyeamrishwa anayeweza kujitenga nayo. Kwa hivyo, hakuumba chochote isipokuwa kwa hekima, na wala hakuamrisha kitu ila kwa hekima. Na hekima ni kukiweka kitu katika mahali pake panapostahiki. Hivyo basi, wao (Malaika) wakakiri na kukubali elimu ya Mwenyezi Mungu na hekima yake, na kushindwa kwao kujua hata kitu kidogo zaidi, na wakakubali fadhila za Mwenyezi Mungu juu yao, na yeye kuwafunza wao wasiyoyajua.