انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٠

يَكَادُ ٱلْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَـٰرَهُمْ ۖ كُلَّمَآ أَضَآءَ لَهُم مَّشَوْا۟ فِيهِ وَإِذَآ أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا۟ ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَـٰرِهِمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ ٢٠

(20) "Kila ukiwatolea mwangaza" yani umeme huo katika giza hizo. "Wanatembea ndani yake. Na linapowawia giza, wanasimama." Yani wanaacha kutembea. Na hivi ndivyo ilivyo hali ya wanafiki wanapoisikia Qur-ani na maamrisho yake na makatazo yake, na ahadi zake na vitisho vyake, wanatia vidole vyao katika masiki yao. Na wanayapa mgongo maamrisho yake na makatazo yake, na ahadi zake, na vitisho vyake. Kwa hivyo, vitisho hivyo vyake vinawatia hofu, na ahadi zake zinawasumbua. Kwa hivyo, wanajiepusha nazo kadiri wawezavyo, na wanazichukia kama vile yule wa mvua anayesikia radi; kwa hivyo akatia vidole vyake katika masikio yake mawili kwa kuogopa kifo. Na huyu (wa mvua) huenda akapata usalama. Ama wanafiki, itakuwaje wapate usalama, ilhali Yeye Mtukufu amewazunguka kwa uwezo na elimu? Basi hawawezi kumkwepa, na wala hawawezi kumshinda. Bali anawahifadhia matendo yao, na atawalipa malipo kamili zaidi. Na pindi walipojaribiwa na uziwi, ububu, na upofu (visivyo vya hisia), na wakafungiwa njia za imani, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema "Na angelitaka Mwenyezi Mungu, angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao," yani kihisia. Basi ndani yake kuna kuwahofisha, na kuwatahadharisha dhidi ya adhabu ya duniani, ili wajihadhari, na wakomeke kutokana na baadhi ya maovu yao na unafiki wao. "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." Hakimshindi chochote. Na katika uwezo wake ni kwamba akitaka kitu, anakifanya bila ya kizuizi wala mpinzani. Na katika aya hii na mfano wake, kuna majibu kwa Al-Qadariyya wanaosema kuwa vitendo vyao haviingii katika uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu vitendo vyao ni miongoni mwa mambo yanayoingia katika kauli yake "Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu."