البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّبِعُوا۟ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُوا۟ بَلْ نَتَّبِعُ مَآ أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ ءَابَآءَنَآ ۗ أَوَلَوْ كَانَ ءَابَآؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْـًٔا وَلَا يَهْتَدُونَ ١٧٠
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akatoa habari kuhusu hali ya washirikina wanapoamrishwa kufuata yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake – katika yale yaliyoelezwa hapo awali, - wanajitenga nayo, na wanasema:
“Bali tutafuata tuliyowakuta nayo baba zetu.” Basi wakatosheka tu na kuwafuata baba zao, na wakaacha kuwafuata Manabii, pamoja na kwamba ndio wajinga kuliko watu wote, na wapotofu wao zaidi. Na hii dhana potofu inayotumika kuikataa haki ni dhaifu mno. Na hii ni dalili juu ya kukengeuka kwao kutoka kwenye haki, na kutoitaka kwao, na kutokuwa kwao na uadilifu. Na lau kuwa wangeongoka kwenye uwongofu wao, na nia yao ikawa nzuri, basi kwa hakika ingelikuwa haki ndiyo makusudio yao. Na mwenye kuifanya haki kuwa ndiyo lengo lake, na akapima baina yake na vinginevyo, kwa hakika haki itambainikia bila shaka yoyote, na ataifuata ikiwa yeye ni mwadilifu. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema,