مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَٱعْبُدْهُ وَٱصْطَبِرْ لِعِبَـٰدَتِهِۦ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُۥ سَمِيًّا ٦٥
{65} Kisha akatoa sababu ya upana wa elimu yake na kuwa kutosahau kwake kwamba Yeye ndiye "Mola Mlezi wa mbingu na ardhi." Kwa hivyo, umola wake juu ya mbingu na ardhi, na kwamba viwili hivyo viko katika nidhamu nzuri zaidi iliyo kamili, ambao hauna kughafilika kokote, wala kupuuza, wala ubatili, ni uthibitisho wa uhakika juu ya elimu yake ya kujumuisha kila kitu. Basi usijishughulishe na hayo, bali ishughulishe nafsi yako na yale yanayokufaa na yenye matokeo mazuri kwako, nayo ni kumuabudu Yeye pekee bila ya mshirika yeyote. "Na usubiri katika kumuabudu," na pambana na nafsi yako kwa hilo, na uitekeleze kwa ukamilifu kulingana na uwezo wako. Na katika kushughulika na ibada ya Mwenyezi Mungu kuna liwazo kwa mja dhidi ya mafungamano yote na matamanio. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Wala usivikodolee macho vile tulivyowastarehesha kwavyo baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu katika hivyo..." Mpaka aliposema, "Na waamrishe ahali zako kuswali, na usubiri juu yake..." hadi mwisho wa aya. "Je, unajua chochote kilicho sawa naye?" Yaani, je unajua chochote kilicho sawa na Mwenyezi Mungu, na chenye kufanana naye miongoni mwa viumbe? Na huku ni kuuliza swali kwenye maana ya kukanusha kunakojulikana tu kwa akili. Yaani, hujui yeyote mwenye jina kama lake wala mwenye kufanana naye. Kwa sababu Yeye ndiye Mola Mlezi, na wengineo wanalelewa naye, Muumba na wengineo wameumbwa, Asiyehitaji kwa njia zote, nao wengineo ni wahitaji kwa dhati zao katika njia zote. Yeye ni mkamilifu wa ukamilifu wote katika njia zote, na wasiokuwa yeye ni wapungufu na hawana ukamilifu wowote isipokuwa ule aliowapa Mwenyezi Mungu. Huu ni uthibitisho wa uhakika kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa, na kwamba kumwabudu Yeye ni haki, na kuabudu chochote badala yake ni batili. Na ndiyo maana akatuamrisha tumwabudu Yeye peke yake na kusubiri juu yake, na akatoa sababu ya [hilo] kwamba yeye ni mkamilifu na wa pekee katika ukuu na majina mazuri zaidi.