انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · مريم
السورة ١٩

مريم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٤

وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُۥ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا ٦٤

{64} Siku moja Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – aliona kwamba Jibril, amani ziwe juu yake, hamteremkii mara kwa mara, akamwambia: Lau ungetujia mara nyingi zaidi ya unavyotujia. Hili lilikuwa kutokana na kuwa na shauku yake kubwa juu yake na kuwa kwake mpweke anapoondoka, na ili moyo wake utulie kwa kuteremka kwake. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha kwa ulimi wa Jibril: "Wala hatuteremki isipokuwa kwa amri ya Mola wako Mlezi" nasi wenyewe hatuna lolote katika suala hilo. Akituamrisha, tunaharakisha kutekeleza amri yake wala hatumuasi katika amri yake yoyote. Kama alivyosema juu yao, "hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanatenda wanayoamrishwa." Kwa maana sisi ni waja tu tunaoamrishwa. "Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo." Yaani, ni yake yote mambo yaliyopita, yajayo, na ya sasa katika zama zote na mahali pote. Na ikishabainika kuwa jambo lote ni la Mwenyezi Mungu, na kwamba sisi ni waja tunaoendeshwa, basi jambo hilo linabakia kuwa kati ya je, hekima ya Mwenyezi Mungu inataka liwe, ndiyo alipitishe, au hailitaki, kwa hivyo akalichelewesha? Ndiyo maana akasema, "Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau." Yaani, Mwenyezi Mungu si mwenye kukusahau au kukupuuza. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukukasirikia." Bali Yeye hakuacha kuendelea kuyajali mambo yako, na kukuendesha kufikia malipo yake na mipango yake mizuri. Yaani, ikiwa tutachelewa kuteremka katika wakati uliozoea, basi lisikuhuzunishe hilo wala lisitukie wasiwasi. Na jua ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyetaka hilo. Kwa sababu ana hekima fulani ndani yake.