الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَن يَهْدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِهِۦ ۖ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَّأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَـٰهُمْ سَعِيرًا ٩٧
{97} Yeye aliyetukuka anajulisha kwamba Yeye ndiye Pekee mwenye kuongoa na kupotosha. Kwa hivyo, yeyote ambaye yeye atamuongoa na akamrahisishia yakawa mepesi na akamuepusha na ugumu, basi kwa hakika huyo ndiye aliyeongoka. Na yule ambaye yeye atampotosha na akamuachilia mbali, na kumuachia nafsi yake, basi hana yeyote wa kumwongoa kando na Mwenyezi Mungu, na wala hana mlinzi yeyote wa kumuokoa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu wakati atakapowakusanya juu ya nyuso zao huku wamehizika, ni vipofu na mabubu, hawaoni wala hawasemi. "Na makazi yao ni Jahannamu," ambayo imekusanya kila wasiwasi kubwa, dhiki na adhabu. "Kila ukifanya kuzimika, tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu," wala hawatapumzishwa na adhabu hiyo, wala hawatahukumiwa ili wafe, wala hawatapunguziwa adhabu yake.