الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَإِذَا جَآءَ وَعْدُ أُولَىٰهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَآ أُو۟لِى بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا۟ خِلَـٰلَ ٱلدِّيَارِ ۚ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا ٥
{5} "Na itakapokuja ahadi ya kwanza yake." Yaani, mara ya kwanza kati ya mbili hizo ambazo watafanya uharibifu, yaani, wakati watakapoufanya uharibifu huo, "tutawatumia" kulingana na majaaliwa yaliyoandikwa kabla, na kuwapa mamlaka juu yenu pia kimajaaliwa ya kiadhabu. "Waja wetu wenye nguvu kubwa;" yaani, mashuja, wenye idadi kubwa na maandalizi mazuri, kisha Mwenyezi Mungu atawasaidia dhidi yenu, wawaue, wawateke wana wenu, wapore mali zenu, na wawaingilie "ndani ya majumba." Kwa hivyo waharibu nyumba hizo, waingie katika Msikiti Mtakatifu, na wauharibu. "Na hii ilikuwa ahadi iliyotimizwa" ambayo ilikuwa lazima itokee kwa sababu ilipatikana sababu ya kutokea kwake kutoka kwao. Wafasiri walitofautiana kuhusiana na hao waliopewa mamlaka dhidi ya Wana wa Israili, lakini walikubaliana kwamba walikuwa kaumu makafiri ima kutoka katika watu wa Iraq, au Al-Jazira, au sehemu nyingineyo. Mwenyezi Mungu aliwapa mamlaka juu ya wana wa Israili wakati kulikuwa na maasia mengi miongoni mwao na wakaacha sheria zao nyingi na wakavuka mipaka katika ardhi.