الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلِ ٱدْعُوا۟ ٱللَّهَ أَوِ ٱدْعُوا۟ ٱلرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا۟ فَلَهُ ٱلْأَسْمَآءُ ٱلْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَٱبْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ١١٠
{110} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaambia waja wake, "Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Ar-Rahman (Mwingi wa rehema)." Yaani, kwa jina lolote mtakalo katika hayo. "Kwa jina lolote mnalomwita, kwani Yeye ana majina mazuri zaidi." Yaani, hana jina isipokuwa jina zuri tu, ndiyo akataze kwamba msimuombe kwa jina hilo. [Bali] kila jina mtakalomuita kwalo, basi makusudio yatafikiwa. Lakini inafaa zaidi kwamba aombwe kwa jina linalofailiana zaidi na kila hali. "Wala usiswali kwa sauti kubwa mno wala usiifiche kwa sauti ndogo mno." Kwa maana, kila moja ya mawili hayo yamekatazwa. Ama kuswali kwa sauti kubwa mno, wakati washirikina wanaoikadhibisha Qur-ani watakapoisikia, wataitukana na kumtukana pia aliyeileta. Na ama kuswali kwa sauti ya chini mno, basi hilo haliwezi kufikisha katika makusudio kwa atakayetaka kuisikia. "Bali shika njia ya kati na kati ya hizo."