النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
خَلَقَ ٱلْإِنسَـٰنَ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ ٤
{4} Na alipotaja kuumbwa kwa mbingu [na dunia], akataja kuumbwa kwa vile vilivyo ndani ya viwili hivyo, na akaanza kwa kitukufu zaidi kati ya hivyo, ambacho ni mwanadamu, akasema: "Amemuumba mtu kwa tone la manii" na akaendelea kuliendesha na kulipandisha, na kulikuza mpaka likawa mwanadamu mkamilifu wa viungo vya nje na vya ndani. Na akamfunika kwa neema zake nyingi mpaka anapokamilika, anajifahiri na nafsi yake na kujiona. "Na tazama, akawa mshindani aliye dhahiri." Inawezekana kwamba kinachomaanishwa ni kuwa yeye anakuwa mshindani wa Mola wake Mlezi, kwa kumkufuru, na kujadiliana na Mitume wake, na anakadhibisha ishara zake, na anasahau uumbaji wake wa kwanza, na neema ambazo Mwenyezi Mungu alimneemesha, naye akazitumia katika kumuasi. Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu kutokana na tone la manii, kisha akaendelea kumhamisha kutoka katika hatua moja hadi nyingine, mpaka alipokuwa na akili timamu, mwenye ubongo na maoni, akaanza kubishana na kujadiliana na Mola wake Mlezi. Basi na mja amshukuru Mola wake Mlezi ambaye alimfikisha katika hali hii, ambayo yeye mwenyewe hawezi kufanya chochote katika hayo.