النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ ۚ تَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ٣
Kisha akataja ushahidi na hoja mbalimbali juu ya hilo, kwa hivyo akasema:
Sura hii inaitwa Sura ya neema. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alitaja mwanzoni mwake misingi ya neema na kanuni zake, na mwishowe akataja vyenye kuzitimiza na kuzikamilisha.
{3} Kwa hivyo akajulisha kwamba "Ameziumba mbingu na dunia" ili waja watumie hilo kama ushahidi juu ya ukuu wa Muumba wake, na sifa zake za ukamilifu. Na wajue kwamba aliziumba ili ziwe makao ya waja wake wanaomwabudu kwa kile anachowaamuru miongoni mwa sheria mbalimbali, ambazo aliziteremsha juu ya ndimi za Mitume wake. Na kwa sababu hiyo akajitakasa kutokana na shirki na wale wanaomshirikisha, akasema: "Ametukuka na hayo wanayoshirikisha nayo." Yaani, ametakasika na ni mkuu mno kuhusishwa na ushirikina wao huo. Kwa maana Yeye ndiye Mungu wa haki, ambaye ibada, upendo, na unyenyekevu havifai kufanywa isipokuwa kwa ajili yake tu.