انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ابراهيم
السورة ١٤

ابراهيم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٩

أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ ١٩

{19} Yeye Mtukufu anawatanabahisha waja wake kwamba "aliziumba mbingu na ardhi kwa Haki." Yaani, ili viumbe vimuabudu Yeye, vimjue, aviamrishe na avikataze, na ili vitumie hayo yaliyomo ndani yake kuwa ni ushahidi juu ya sifa zake kamilifu, na ili wajue kwamba yule aliyeziumba mbingu na ardhi - pamoja na ukubwa wake na upana wake - ana uwezo wa kuwarejesha katika uumbaji mpya, ili awalipe kwa uzuri wao na ubaya wao, na kwamba uwezo wake na utashi wake hauwezi kushindwa hayo. Na ndiyo maana akasema: "Akitaka, anawaondoa na alete viumbe wapya!" Inawezekana kwamba maana yake ni kuwa akitaka anawaondoa na alete kaumu wengine wasiokuwa nyinyi, ambao watakuwa watiifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko nyinyi. Na inawezekana kwamba kinachokusudiwa ni kuwa akitaka, anawaangamiza kisha awarudishe kama viumbe wapya kwa kuwafufua. Na uwezekano huu unaashiriwa na yale aliyotaja baada yake kuhusu hali za Qiyama.