يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالُوٓا۟ إِن يَسْرِقْ فَقَدْ سَرَقَ أَخٌ لَّهُۥ مِن قَبْلُ ۚ فَأَسَرَّهَا يُوسُفُ فِى نَفْسِهِۦ وَلَمْ يُبْدِهَا لَهُمْ ۚ قَالَ أَنتُمْ شَرٌّ مَّكَانًا ۖ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا تَصِفُونَ ٧٧
77. Basi ndugu zake Yusuf walipoona yale waliyoona; "Wakasema: Akiiba huyu” ndugu yetu, basi hili si jambo geni kwake, "basi hakika nduguye vile vile aliiba hapo zamani” wakimaanisha Yusuf, amani iwe juu yake, na makusudio yao kwa hilo ni kujiondoa lawamani, na kwamba huyu na nduguye wanaweza kuiba, na wao si ndugu zetu wa kwa baba na mama. Na katika hili kuna kuwapuuza kukubwa, na ndiyo maana "Yusuf akaliweka hilo kisiri katika moyo wake wala hakulionyesha kwao.” Yaani, hakuwajibu kwa sababu ya hayo waliyoyasema kwa wanayoyachukia, bali aliizuia hasira yake na akalificha jambo hilo ndani ya nafsi yake, na “akasema” katika nafsi yake “Nyinyi ndio mko katika hali paovu zaidi” kwa kuwa mmetushutumu kwa yale ambayo nyinyi mko katika yaliyo maovu zaidi yake. "Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayosingizia” kuhusiana nasi kwa wizi mnaotutuhumu kwao ambao Mwenyezi Mungu anajua kwamba hatuna hatia yoyote katika hilo.