يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَبَدَأَ بِأَوْعِيَتِهِمْ قَبْلَ وِعَآءِ أَخِيهِ ثُمَّ ٱسْتَخْرَجَهَا مِن وِعَآءِ أَخِيهِ ۚ كَذَٰلِكَ كِدْنَا لِيُوسُفَ ۖ مَا كَانَ لِيَأْخُذَ أَخَاهُ فِى دِينِ ٱلْمَلِكِ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَـٰتٍ مَّن نَّشَآءُ ۗ وَفَوْقَ كُلِّ ذِى عِلْمٍ عَلِيمٌ ٧٦
{76} Basi mkaguzi huyo akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa ndugu yake, ili iondoke shaka ya kufikiriwa kwamba hilo lilifanywa kimakusudi. Na wakati hakupata chochote katika mizigo yao, "akalitoa katika mzigo wa nduguye” na hakusema: alilipata au ndugu yake aliliiba, kwa kuzingatia ukweli halisi. Basi hapo Yusuf akatimiza alichotaka kwamba ndugu yake abaki pamoja naye kwa njia ambayo ndugu zake hawawezi kuhisi. Akasema Yeye Mtukufu: "Hivyo ndivyo tulivyompangia njama Yusuf” Yaani, tulimrahisishia njama hii, ambayo kwayo alifikia jambo ambalo si la kulaumiwa. "Hakuwa ni wa kumzuia nduguye kwa sheria ya mfalme huyo” kwa sababu si katika sheria yake kuwa mwizi amilikiwe, bali wao wana malipo mengine. Na ikiwa hukumu ya hilo ingerudishwa katika sheria ya mfalme huyo, basi Yusuf hangeweza kumbakisha nduguye pamoja naye, lakini alifanya wao wenyewe wapitishe hukumu hiyo ili kitimie kile alichotaka. Yeye Mtukufu alisema "Tunamuinua daraja tumtakaye” kwa elimu yenye manufaa na kujua njia zinazofikisha kwenye makusudio yake, kama tulivyoinua daraja za Yusuf. "Na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.” Kwa hivyo, kila ajuaye juu yake kuna yule ambaye anajua zaidi yake mpaka elimu yote iishie kwa Mwenye kujua ya ghaibu na yanayoonekana.