انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٣

فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيْنَـٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِى ٱلْفُلْكِ وَجَعَلْنَـٰهُمْ خَلَـٰٓئِفَ وَأَغْرَقْنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُنذَرِينَ ٧٣

{73} "Lakini wakamkadhibisha" baada ya kuwalingania usiku na mchana, kwa siri na hadharani, lakini kulingania kwake huko hakukuwazidishia isipokuwa kukimbia. "Kwa hivyo tukamwokoa, pamoja na wale waliokuwa naye, katika jahazi," ambalo tulimwamrisha alijenge mbele ya macho yetu, na tukamwambia, "Tanuri itakapofoka maji, basi beba humo kwa jozi dume na jike kutoka kwa kila aina, na ahali zako, isipokuwa wale ambao imekwisha tangulia kauli juu yao, na wale walioamini." Kwa hivyo, akafanya hivyo, basi Mwenyezi Mungu akaamrisha mbingu kumimina maji, na tukaipasua ardhi kwa chemchemi. Kwa hivyo, maji hayo yakakutana kwa jambo lililokwishapitishwa. Na tukambeba kwenye safina ya mbao na kamba, ikawa inakwenda mbele ya macho yetu. "Na tukawafanya wao ndio waliobakia" katika ardhi baada ya kuwaangamiza waliokadhibisha. Kisha Mwenyezi Mungu akabariki katika dhuria yake na akawafanya dhuria wake ndio wenye kubakia, na akawaeneza katika pande za ardhi, "na tukawazamisha wale waliozikadhibisha Ishara zetu" baada ya kubainisha huko na kusimamisha ushahidi. "Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa." Nao ulikuwa maangamizo ya kuhizi, na laana ya kufuatana juu yao katika kila kizazi kitakachokuja baada yao. Hakitasikia kuwahusu isipokuwa lawama tu, wala hakitaona isipokuwa shutuma na kashfa. Basi na wajitahadhari hawa wanaokadhibisha yasije yakawapata yale yaliyowapata wale kaumu waliokadhibisha ya maangamizo, hizaya, na adhabu.