يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ ٱلْمُسْلِمِينَ ٧٢
{72} Ndiyo maana akasema: "Na mkigeuka" mkayaacha yale niliyowalingania kwayo, basi hakuna sababu kwa kugeuka kwenu huko. Kwa sababu, imebainika kwamba nyinyi hamgeuki kutoka kwenye batili kwenda kwenye haki; bali mnageuka kutoka kwenye haki ambayo ushahidi ulisimama juu ya usahihi wake kwenda kwenye batili ambayo ushahidi ulisimama juu ya uharibifu wake. Lakini pamoja na haya, "mimi sikuwaomba ujira wowote" juu ya ulinganizi wangu na juu ya kuitikia kwenu ndiyo mseme: Huyu ametujia ili achukue mali zetu, kwa hivyo mkakataa kwa sababu ya hili. "Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu." Yaani, sitaki thawabu na malipo isipokuwa kutoka Kwake. "Na" pia mimi hakika sikuwaamrisha jambo fulani, kisha nikawahalifu kwenda kinyume nalo. Bali "nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu;" basi mimi ndiye wa kwanza kuingia na wa kwanza kufanya kile nilichowaamrisha.