يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ إِذْنِهِۦ ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ فَٱعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ٣
{3} Yeye Mtukufu Anasema akibainisha umola wake, uungu wake, na ukuu wake, “Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita” pamoja na kwamba anaweza kuziumba kwa muda mfupi sana, lakini kwa sababu ya hekima yake ya kiungu katika hilo, na kwa sababu Yeye ni mpole katika vitendo vyake. Na katika hekima yake, ndani yake ni kwamba aliziumba kwa haki na kwa ajili ya haki, ili ajulishe kuhusu majina yake na sifa zake, na ili afanyiwe Yeye tu ibada. "Kisha" baada ya kuziumba mbingu na ardhi "akaimarika juu ya Kiti cha Enzi," kuimarika kunakolingana na ukuu wake. "Anaendesha mambo yote” katika ulimwengu wa juu na wa chini, kama vile kufisha na kuhuisha, na kuteremsha riziki, na kubadilisha masiku baina ya watu, na kuondoa madhara kwa wenye shida, na kuitikia maombi ya waombaji. Kwa hivyo, aina mbalimbali za uendeshaji vinashuka kutoka kwake na kupanda kwake, na viumbe vyote vinanyenyekea kwa utukufu wake na viko chini ya ukuu na mamlaka yake. "Hakuna mwombezi yeyote isipokuwa baada ya idhini yake.” Basi hakuna hata mmoja miongoni mwao anayeweza kuanza kufanya uombezi hata kama yeye ndiye mbora wa viumbe vyote mpaka Mwenyezi Mungu ampe idhini, na wala humpi idhini isipokuwa yule anayemridhia, na wala hawaridhii isipokuwa wenye ikhlasi na kumpwekesha Yeye. "Huyo" ambaye yuko hivi "ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi.” Yaani, Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye ambaye ana sifa ya uungu, ambayo inajumuisha sifa za ukamilifu, na sifa ya umola inayojumuisha sifa za matendo. "Basi mwabuduni yeye." Yaani, mpwekesheni kwa yote mnayoweza miongoni mwa aina mbalimbali za uja. “Je, hamkumbuki?” Ushahidi mbalimbali unaoashiria kuwa Yeye pekee ndiye aabudiwaye, Msifiwa, Mwenye utukufu na heshima.