At-Tawba
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَـٰجِدَ ٱللَّهِ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا ٱللَّهَ ۖ فَعَسَىٰٓ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَن يَكُونُوا۟ مِنَ ٱلْمُهْتَدِينَ 18
{18} Kisha akataja ni nani wanaoiimarisha misikiti ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo akasema: "Hakika anayeimarisha tu misikiti ya Mwenyezi Mungu ni yule anayemwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akasimamisha Sala" za wajibu na zile zinazopendekezwa, kwa kusimamisha kwa dhahiri yake na ndani, "na akatoa Zaka" akawapa wastahiki wake. "Na wala hakumnyenyekea isipokuwa Mwenyezi Mungu." Yaani alikufanya kunyenyekea kwake kwa ajili ya Mola wake Mlezi tu, kwa hivyo akaacha yale ambayo Mwenyezi Mungu aliharamisha, na wala hakupunguza haki za Mwenyezi Mungu za lazima. Kwa hivyo aliwaelezea kuwa wana imani yenye manufaa, na kufanya matendo mema ambayo mama yake ni sala, na Zaka, na kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, ambako ndiko msingi wa kila heri. Basi hawa ndio wanaoiimarisha misikiti kwa uhakika, na ndio wenyewe ambao ndio wastahiki wake. "Basi huenda hao wakawa katika waongofu." Na "huenda" kama inahusu Mwenyezi Mungu, basi ni lazima ifanyike. Na ama yule ambaye hakumwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala hamnyenyekei Mwenyezi Mungu, basi huyu si katika wale wanaoiimarisha misikiti ya Mwenyezi Mungu, wala si katika wenyewe ambao ndio wastahiki wake, hata kama watafikiri hivyo na kudai hivyo.