سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Fajr
سورت 89

Al-Fajr

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیات 6–14

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ 6 إِرَمَ ذَاتِ ٱلْعِمَادِ 7 ٱلَّتِى لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِى ٱلْبِلَـٰدِ 8 وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُوا۟ ٱلصَّخْرَ بِٱلْوَادِ 9 وَفِرْعَوْنَ ذِى ٱلْأَوْتَادِ 10 ٱلَّذِينَ طَغَوْا۟ فِى ٱلْبِلَـٰدِ 11 فَأَكْثَرُوا۟ فِيهَا ٱلْفَسَادَ 12 فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ 13 إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلْمِرْصَادِ 14

{6 - 14} Mwenyezi Mungu anasema: "Kwani hukuona" kwa moyo wako na ufahamu wako, "jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya" mataifa haya dhalimu, ambayo ni 'Adi ambayo ndio "Iram" ambao ni kabila maarufu huko Yemeni "wenye majumba marefu" na nguvu iliyokithiri na kiburi. "Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?" Kwa sababu ya nguvu zao na ukali wao; kama alivyowaambia Nabii wao Hud - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - "Na kumbukeni alivyokufanyeni mshike pahala pa kaumu ya Nuhu, na akakuzidisheni katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa." Na akasema "Na Thamudi waliochonga majabali huko bondeni?" Yaani: bonde la Al-Qura. Walikuwa wakichonga majabali kwa nguvu zao, na wakayafanya kuwa maskani yao. "Na Firauni mwenye vigingi?" Yaani, mwenye askari waliouimarisha ufalme wake kama vile vigingi vinavyoimarisha kile ambacho vinashikilia. "Ambao walifanya jeuri katika nchi?" Maelezo haya yanawahusu akina Adi, Thamudi, Firauni na wale waliowafuata. Hao walifanya jeuri katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, na wakawadhuru waja wa Mwenyezi Mungu katika dini yao na dunia yao. Ndiyo maana akasema: "Wakakithirisha humo uharibifu?" Nao ni ukafiri na matawi yake ya kila aina ya maasia, na wakajitahidi kupigana vita na Mitume na kuwazuilia watu njia ya Mwenyezi Mungu. Lakini walipofika kiwango cha uasi ambacho kililazimu waangamizwe, Mwenyezi Mungu akawaletea mjeledi wa adhabu. "Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia" kwa mwenye kumuasi. Yeye humpa muda kidogo, kisha mchukue amshike mshiko wa Mwenye nguvu Mwenye uwezo mno.