An-Naazi'aat
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
ءَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُ ۚ بَنَىٰهَا 27 رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّىٰهَا 28 وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَىٰهَا 29 وَٱلْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ 30 أَخْرَجَ مِنْهَا مَآءَهَا وَمَرْعَىٰهَا 31 وَٱلْجِبَالَ أَرْسَىٰهَا 32 مَتَـٰعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَـٰمِكُمْ 33
{27 - 33} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, akiwabainishia ushahidi wazi wale wanaokanusha ufufuo na wanaokataa suala la Mwenyezi Mungu kurejesha miili: "Je, ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi" watu "au mbingu" zenye maumbile makubwa, ya nguvu, zilizoinuka juu sana? "Yeye" Mwenyezi Mungu "ndiye aliyeijenga! Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri" na ukamilifu wa hali ya juu unaozichanganya akili na kuzishangaza nyoyo. "Na akautia giza usiku wake" nalo likatanda pande zote za mbingu, kwa hivyo uso wa ardhi ukawa giza. "Na akautokeza mchana wake" jua lilipochomoza, kwa hivyo watu wakaenea kwa ajili ya masilahi ya dini yao na dunia yao. "Na juu ya hivyo" baada ya kuumbwa mbingu "ameitandaza ardhi" na kutia humo manufaa yake, kama alivyofasiri hilo kwa kauli yake: "Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake. Na milima akaisimamisha imara." Na suala la kuitandaza ardhi kulikuwa baada ya kuumba mbingu. Kama ilivyo katika maandiko ya Aya hizi tukufu. Na ama kuumbwa kwa ardhi yenyewe, huko kulitangulia kuumbwa mbingu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliyeumba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote..." mpaka aliposema: "Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa hiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu. Basi akazifanya mbingu saba..." Kwa hivyo, yule aliyeziumba mbingu kubwa na mianga na miili iliyomo ndani yake, na ardhi yenye mavumbi na nene, na mahitaji ya lazima na manufaa ya viumbe, ni lazima atawafufua viumbe waliojukumishwa kisheria ili awalipe kwa matendo yao. Kwa hivyo, aliyefanya wema, basi atalipwa na wema. Naye aliyefanya ubaya, basi kamwe asilaumu isipokuwa yeye mwenyewe tu.