سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Muddaththir
سورت 74

Al-Muddaththir

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیات 11–30

ذَرْنِى وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا 11 وَجَعَلْتُ لَهُۥ مَالًا مَّمْدُودًا 12 وَبَنِينَ شُهُودًا 13 وَمَهَّدتُّ لَهُۥ تَمْهِيدًا 14 ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ 15 كَلَّآ ۖ إِنَّهُۥ كَانَ لِـَٔايَـٰتِنَا عَنِيدًا 16 سَأُرْهِقُهُۥ صَعُودًا 17 إِنَّهُۥ فَكَّرَ وَقَدَّرَ 18 فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ 19 ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ 20 ثُمَّ نَظَرَ 21 ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ 22 ثُمَّ أَدْبَرَ وَٱسْتَكْبَرَ 23 فَقَالَ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ 24 إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا قَوْلُ ٱلْبَشَرِ 25 سَأُصْلِيهِ سَقَرَ 26 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا سَقَرُ 27 لَا تُبْقِى وَلَا تَذَرُ 28 لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ 29 عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ 30

{11 - 30} Aya hizi ziliteremshwa kuhusu Al-Walid bin Al-Mughirah, ambaye alikuwa mkaidi dhidi ya haki, na ambaye alisimama kukabiliana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kupigana naye na kumpinga. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamkashifu kwa kashfa ambayo hakuwahi kumkashifu mwingineye. Na haya ndiyo malipo kwa wote wanaoikaidi haki na kupingana nayo; kwamba atapata hizaya katika dunia, na tena adhabu ya Akhera ni ya kufedhehesh zaidi. Akasema: "Niache peke yangu na niliyemuumba" Yaani: Nilimuumba peke yake, bila ya mali, familia, wala mtu mwingine yeyote. Basi nikaendelea kumlea na kumpa, na nikamjaalia "awe na mali nyingi na" pia nikamfanyia kuwa na "wana" wa kiume "wanaoonekana" Yaani: waliopo pamoja naye daima, anawafurahia, hutimiza haja zake kupitia kwa hao, na kutafuta msaada kupitia kwao "Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa" katika dunia na sababu zake mpaka yakatekelezeka mambo anayotafuta na kutamani. "Kisha" pamoja na neema hizi na hivi vyote alivyopewa "anatumai nimzidishie!' Yaani anatazamia kupata neema za Akhera kama alivyozipata neema za dunia. "Hasha!" Yaani jambo hili si kama alivyokuwa akitaka, bali ni kinyume na aliyoyakusudia na kuyataka. Na hayo ni "kwa sababu hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!" Alizijua kisha akazikanusha, na zikamwita kwenye haki, lakini hakunyenyekea kwazo, na bado haikumtosha kujiepusha nazo na kuzipa mgongo. Bali alianza kupigana nao vita na kujitahidi kuzibatilisha, na ndiyo maana akasema juu yake: "Kwani hakika yeye alifikiri" ndani ya nafsi yake "na akapima" kile alichofikiria ili aseme kauli atakayoibatilisha Qur-ani kwayo. "Basi ameangamia! Vipi alivyopima! Tena ameangamia! Vipi alivyopima!" Kwa sababu alipima kitu kisichokuwa ndani ya upeo wake, na akajiingiza katika kile ambacho yeye wala mfano wake hawawezi kukifikia. "Kisha akatazama" cha kusema "kisha akakunja kipaji, na akanuna" ili kuikimbia kuichukia haki. "Kisha akaipa kisogo haki" na akaenda zake "na akatakabari" hili likiwa ni matokeo ya juhudi zake za kiakili, kivitendo na kwa maneno. "Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa. Haya si chochote ila kauli ya binadamu." Yaani, haya si maneno ya Mwenyezi Mungu. Bali ni maneno ya wanadamu, na pia si maneno ya wanadamu wema, bali ni maneno ya waovu miongoni mwao na wasiomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa kila mwongo na mchawi, basi naangamie! Jinsi gani alivyo mbali mno zaidi na usahihi! Na ni mwenye kustahili zaidi vipi hasara na kuangamia! Je, inawezaje kuingia katika akili ya mtu yeyote au kufikiriwa na dhamiri ya mtu yeyote kwamba maneno ya juu kabisa na makuu zaidi, maneno ya Mola Mlezi, Mtukufu, Mwenye heshima, Mkuu kwamba yanafanana na maneno ya viumbe maskini, wapungufu?! Au huyu mwongo mkaidi anathubutu vipi kuelezea maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa maelezo haya? Hastahiki chochote ila adhabu kali [na mateso mazito], na ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. Na ni nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? Haubakishi wala hausazi" mwenye kuadhibiwa. "Unababua mno ngozi iwe nyeusi." Yaani, unawababua na kuwaingiza mno katika adhabu yake, na unawatia wasiwasi kwa ukali wa joto lake na baridi yake kali. "Juu yake wapo kumi na tisa" miongoni mwa Malaika, wasimamizi wake, wakali na wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu katika anayowaamrisha na wanafanya wanayoamrishwa.