As-Saff
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَإِذْ قَالَ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ يَـٰبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ إِنِّى رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَىَّ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ وَمُبَشِّرًۢا بِرَسُولٍ يَأْتِى مِنۢ بَعْدِى ٱسْمُهُۥٓ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ قَالُوا۟ هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ 6
{6} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akieleza kuhusu ukaidi wa Wana wa Israili waliotangulia, ambao Isa bin Maryamu aliwalingania na kuwaambia: “Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu.’” Yaani, Mwenyezi Mungu alinituma ili nikuiteni kwenye heri na kukukatazeni maovu, na akaniunga mkono kwa hoja zilizo wazi, na katika yale yanayoonyesha ukweli wangu ni kuwa “ninayathibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati.” Yaani, Nimeleta yale aliyoyaleta Musa katika Taurati na sheria za mbinguni, kama mimi ningekuwa ninadai tu kwamba mimi ni Nabii, ilhali si Nabii, basi ningekuja na kisichokuwa kile walichokuja nacho Mitume waliotangulia, na “ninayathibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati” pia ni kwamba kitabu hicho kilitoa habari na bishara njema ya kuja kwangu, nimi nimetumwa ili kusadikisha hilo, “na kubashiria kuja Mtume atakayekuja baada yangu; jina lake ni Ahmad!” Naye ni Muhammad bin Abdullah bin Abdul Muttalib Nabii wa kabila la Hashim. Basi Isa, rehema na amani ziwe juu yake, ni kama manabii wengine wote. Anamsadiki nabii aliyetangulia, na anapeana bishara njema ya nabii atakayekuja baadaye. Tofauti na waongo; Kwani wao wanapingana na Manabii vikali zaidi, na wanahitalifiana nao kwa maelezo, maadili, maamrisho na makatazo. “Lakini alipowajia;” yaani, Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ambaye Isa alipeana bishara njema ya kuja kwake “na hoja zilizo wazi.” Yaani, ushahidi wa wazi wenye kuwaonyesha kwamba yeye ndiye, na kwamba hakika yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, “wakasema” wakiikaidi na kukadhibisha haki: “Huu ni uchawi ulio dhahiri!” Na hili ni katika maajabu makubwa zaidi. Mtume ambaye ujumbe wake umekwisha dhihirika zaidi kuliko jua la mchana, anafanywa kuwa mchawi ambaye uchawi wake uko wazi. Je, kuna kuachiliwa mbali kukubwa zaidi kuliko huku? Je, kuzulia uongo kukubwa zaidi kuliko kuzulia huku, ambako kunamkanushia yale yaliyokuwa yanajulikana kwake ya ujumbe wake na kumthibitishia yale ambayo yeye ndiye mtu wa mbali zaidi nayo kuliko watu wote?