Al-An'aam
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَوَهَبْنَا لَهُۥٓ إِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُۥدَ وَسُلَيْمَـٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ 84
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomtaja mja wake na rafiki mwandani wake Ibrahim, amani iwe juu yake, na akataja yale aliyomneemesha kwayo ya elimu, na kulingania, na subira. Akataja yale ambayo Mwenyezi Mungu alimtukuza kwayo miongoni mwa dhuria njema, na kizazi kizuri, na kwamba Mwenyezi Mungu alimweka aliye bora zaidi wa viumbe vyote kutoka katika kizazi chake. Basi ni kukubwa kulioje hadhi hii, heshima kubwa ambayo haina mfano wake! Kwa hivyo, Akasema:
{84} "Na tukamtunuku (Ibrahim) Is-haq na Yaakub," mwanawe ambaye ndiye Israili, baba wa mataifa ambaye Mwenyezi Mungu alimfadhilisha juu ya walimwengu wote. "Kila mmoja wao" katika wawili hao tulimuongoa kwenye njia iliyonyooka katika elimu yake na vitendo vyake. Na "Nuhu" tulimuongoa "kabla," na uwongofu wake ni miongoni mwa uwongofu wa juu zaidi maalumu ambao haukuwahi kufanyika isipokuwa tu kwa watu fulani tu miongoni mwa walimwengu. Nao ni wale wenye stahamala kubwa miongoni mwa Mitume ambao yeye ni miongoni mwao. "Na katika dhuria zake," inawezekana kwamba neno hili (yake) linamrejea Nuhu. Kwa sababu yeye ndiye aliyetajwa mwisho, na kwa sababu Mwenyezi Mungu alimtaja Lut’ pamoja na wale aliowataja, naye ni katika dhuria ya Nuhu, na si katika dhuria ya Ibrahim. Kwa sababu yeye ni kijana wa kaka yake (Nuhu). Na inawezekana kwamba neno hilo (yake) linamrudia Ibrahim. Kwa sababu muktadha huu ni katika kumsifu. Na Lut, ijapokuwa si katika kizazi chake, lakini alikuwa miongoni mwa wale walioamini kupitia mkononi mwake, kwa hivyo hadhi yake na fadhila yake Al-Khalil ikawa kubwa zaidi kuliko ile ya kuwa kwake mwanawe tu. "Na Daudi na Suleman" mwana wa Daud, "na Ayyub na Yusuf" mwana wa Yaakub, "na Musa na Harun" wana wa ‘Imran. "Na hivi ndivyo" kama tulivyowafanya dhuria ya Ibrahim Al-Khalil kuwa wema. Kwa sababu alimuabudu Mola wake Mlezi kwa uzuri, na akafanya uzuri katika kuwanufaisha viumbe, basi vivyo hivyo ndivyo "tunavyowalipa wafanyao mazuri" kwa kuwapa sifa njema ya ukweli, na dhuria njema kulingana na kufanya kwao mazuri.