Al-An'aam
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا۟ كُلَّ ءَايَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا۟ بِهَا ۚ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُوكَ يُجَـٰدِلُونَكَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّآ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ 25
{25} Yaani, miongoni mwa washirikina hawa wamo kaumu ambao nyakati fulani wanafanywa na mambo fulani kusikiliza [unayoyasema], lakini huko ni kusikiliza bila kukusudia haki na kuifuata. Na ndiyo maana hawanufaiki na kusikiliza huko kwa sababu ya kutotaka kwao heri. "Na tumezitia pazia kwenye nyoyo." Yaani, vya kuifunika na vigubiko ili wasielewe maneno ya Mwenyezi Mungu, hivyo basi akayalinda maneno Yake dhidi ya mfano wa hawa. "Na masikioni mwao" tukatia "uziwi." Basi hawasikii cha kuwanufaisha "na wakiona kila Ishara, hawaiamini." Na huu ndio udhalimu wa mwisho na ukaidi, kwamba Aya zilizo wazi zenye kuonyesha kwenye haki hawazifuati wala hawazisadiki, bali wao wanaijadili haki kwa batili ili waikanushe. Na kwa sababu ya hayo akasema, "Mpaka wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema wale waliokufuru: Hizi si chochote isipokuwa hadithi za watu wa kale. Yaani, yamechukuliwa kutoka katika maandishi ya watu wa kale ambayo hayatokani na Mwenyezi Mungu wala Mitume wake. Na huu ni katika kufuru yao, vinginevyo, basi vipi kitabu hiki chenye habari za waliokuja kabla na baada yao, na mambo ya uhakika ambayo walikuja nayo Manabii na Mitume, na haki, na uadilifu kamili katika kila namna yanaweza kuwa ngano za watu wa kale?