Al-An'aam
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
قُلْ فَلِلَّهِ ٱلْحُجَّةُ ٱلْبَـٰلِغَةُ ۖ فَلَوْ شَآءَ لَهَدَىٰكُمْ أَجْمَعِينَ 149
{149} Na miongoni mwake ni kuwa, hoja ni ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni ya kukata, ambayo hakubaki yeyote na udhuru wowote, na ambayo walikubaliana juu yake Manabii na Mitume, na Vitabu vya Mwenyezi Mungu, na hadithi za unabii, na akili timamu, na umbile la asili lilionyooka, na maadili mema. Kwa hivyo, ikajulikana kwa hilo kuwa kila kitu kinachopingana na aya hii ya mkato ni batili. Kwa sababu kinyume cha haki hakiwi isipokuwa batili. Na miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa kila kiumbe uwezo na utashi anayoweza kwayo kufanya kile alichoamrishwa kufanya. Na Mwenyezi Mungu hakumlazimisha yeyote kufanya kile asichoweza, kufanya, wala hakumharamishia yeyote kile asichoweza kukiacha. Basi kutumia majaliwa na matokea yake kama hoja baada ya hayo, ni dhuluma tupu na ukaidi mtupu. Na miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwalazimisha waja wake kufanya vitendo vyao. Bali aliyafanya matendo yao kufuatana na chaguo lao. Wakitaka, wanafanya, na wakitaka wanaacha. Na hili ni jambo linaloshuhudiwa na halikatai isipokuwa mwenye kiburi na akayakataa mambo ya hisia. Kwa maana kila mwenye kutofautisha kati ya harakati za hiari na harakati za kulazimishwa, ingawa zote hizo zinaingia katika mapenzi ya mwenyezi Mungu na yako chini ya kutaka kwake. Na miongoni mwake ni kwamba, wale wanaotumia majaliwa na matokeo yake juu ya kufanya maasia wanapingana katika hilo. Kwani hawawezi kuitumia katika kila hali. Bali lau kama mkosaji angewafanyia kosa kwa kuwapiga au kuchukua mali yao au mfano wa hayo, na akatumia majaliwa ya Mwenyezi Mungu na matokeo yake kuwa hoja yake, hawangekubali hoja hii kutoka kwake, na wangekasirika sana juu ya hilo. Basi ee maajabu haya! Vipi wanaitumia kama hoja juu ya kumuasi mwenyezi Mungu, na machukizo yake, wala hawakubali kwa yeyote kuitumia kama hoja yake dhidi ya yale yenye kuwakasirisha? Na miongoni mwake ni kwamba, kutumia majaliwa na matokeo yake kama hoja siyo makusudio yao, na wanajua vyema kuwa si hoja. Bali makusudio katika hilo ni kuipinga haki, na wanaona kuwa haki iko sawa na kitu kipya kilichowaingilia. Kwa hivyo wanaizuia kwa kila kitu kinachokuja akilini mwao miongoni mwa maneno [hata kama wanaitakidi kuwa ni kosa].