سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
سورت 6

Al-An'aam

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 138

وَقَالُوا۟ هَـٰذِهِۦٓ أَنْعَـٰمٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَآ إِلَّا مَن نَّشَآءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَـٰمٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَـٰمٌ لَّا يَذْكُرُونَ ٱسْمَ ٱللَّهِ عَلَيْهَا ٱفْتِرَآءً عَلَيْهِ ۚ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ 138

{138} Na katika aina za upumbavu wao ni kuwa mifugo ambao Mwenyezi Mungu aliwahalalishia kwa ujumla na akawafanya kuwa riziki na rehema ili wafurahie kwayo na kunufaika nao, walizua ndani yake uzushi na maneno yao wenyewe. Wana maneno waliyokubaliana juu yake katika baadhi ya mifugo na mimea kwamba wanasema kuyahusu kuwa: "Mifugo hawa na mimea ni miiko." Yaani, vimeharamishwa, hawavili "isipokuwa tumtakaye;" yaani, hairuhusiki kwa yeyote kuvila isipokuwa yule tunayemtaka avile au tunayemueleza kwa maelezo yetu wenyewe. Na yote haya ni kwa madai yao tu, hayana msingi wowote wala hoja isipokuwa matamanio yao na maoni yao wenyewe mapotofu. Na mifugo wengine ambao si haramu kwa njia zote, bali wanaharamisha migongo yao tu. Yaani, kwa kuwapanda na kubeba juu yao, na wanailinda migongo yao, na wanawaita Al-Ham. Na mifugo wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao, bali wanayataja juu yao majina ya masanamu yao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na wanayanasibisha matendo hayo kwa Mwenyezi Mungu, lakini wao ni waongo, waovu katika hayo. "Atawalipa kwa hayo ya uwongo waliyokuwa wakiyazua" dhidi ya Mwenyezi Mungu, kama vile kuhalalisha ushirikina na kuharamisha yaliyo halali miongoni mwa vyakula na manufaa mbalimbali.