Al-An'aam
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَجَعَلُوا۟ لِلَّهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ ٱلْحَرْثِ وَٱلْأَنْعَـٰمِ نَصِيبًا فَقَالُوا۟ هَـٰذَا لِلَّهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَآئِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَآئِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى ٱللَّهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَآئِهِمْ ۗ سَآءَ مَا يَحْكُمُونَ 136
{136} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu yale wanayoyafanya washirikina wanaomkadhibisha Nabii -rehema na amani zimshukie – ya upumbavu wa akili, na uhafifu wa maoni, na ujinga mkubwa; na Yeye Mwingi wa baraka, Mtukufu akahesabu baadhi ya itikadi zao potofu. Ili atanabahishe kwa hilo upotovu wao na kutahadharisha nao, na kwamba upinzani wa mfano wa wapumbavu hao kwa haki ambayo ililetwa na Mtume (s.a.w) haiitii dosari hata kidogo. Kwani wao hawana sifa za kuwawezesha kukabiliana na haki, kwa hivyo ikataja katika hayo kuwa, "walimwekea Mwenyezi Mungu" fungu "katika mimea na wanyama aliowaumba," na washirikishwa wao pia wana fungu katika hayo. Na hali ni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyeviumba kwa ajili ya waja wake na akavifanya kuwapo ili iwe riziki kwao. Lakini hao wakajumuisha haramu mbili, na hata haramu tatu. Wao kumtajia Mwenyezi Mungu kwamba walimneemesha kwa kumuwekea fungu pamoja na wao kuitakidi kwamba hilo ni sadaka kutoka kwao. Na kuwashirikisha washirikishwa ambao hawakuwaruzuku wao wala hawakuwapa chochote katika hayo. Na hukumu yao ya dhuluma ambayo ni kwamba vile vilivyokuwa vya Mwenyezi Mungu hawakuvitia maanani wala hawakuvijali, hata ikiwa vitawafikia washirikishwa wao ingawa havikuwa vya washirikishwa wao hao, wanavitunza na kuvihifadhi, na hakuna chochote kwavyo chenye kumfikia Mwenyezi Mungu. Haya ni kwa sababu ikiwa wangepata chochote katika mazao yao, na matunda, na mifugo yao ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumbia, wangekifanya sehemu mbili. Sehemu moja wakasema: Hiki ni cha Mwenyezi Mungu - kwa mujibu wa maneno yao na madai yao. - Vinginevyo; hakika Mwenyezi Mungu hakubali isipokuwa kile kilichokusudiwa kwacho uso wake peke yake, na wala hayakubali matendo ya mwenye kumshirikisha na wengine. Na sehemu nyingine wakaifanya kuwa fungu la washirikishwa wao miongoni mwa vyote viabudiwavyo visivyo Mwenyezi Mungu, na wenza. Basi ikiwa kitu katika vile walivyovifanya kuwa ni vya Mwenyezi Mungu kitafika na kikachanganyika na vile walivyovifanya kuwa ni vya asiyekuwa yeye, hawayajali hayo, na wanasema, “Mwenyezi Mungu hayahitaji;” kwa hivyo, hawaviregeshi. Na kikifika chochote katika vile walivyowawekea miungu wao katika vile walivyomwekea mwenyezi mungu, Wanavirudisha mahali pake, na wanasema: hawa miungu ni wahitaji (masikini), lazima fungu lao lirudishwe. Je, kuna baya zaidi kuliko hukumu hii na yenye dhulma zaidi, kwa vile wanavyoyafanya yale ya kiumbe wanajitahidi ndani yake, na kushauri juu yake, na kuhifadhi zaidi ya yale yanayofanywa katika haki ya Mwenyezi Mungu? Na inawezekana kwamba tafsiri ya Aya hii tukufu kuwa yale yaliyothibiti katika “Sahihi” kutoka kwa Nabii – Rehema na Amani zimshukie – kwamba alisema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa alisema: “Mimi ndiye nisiyehitaji zaidi kuwa na mshirika kati ya washirika. Mwenye kunishirikisha na chochote, ninamuacha yeye na hicho alichoshirikisha ndani yake.” Na kwamba, maana ya Aya ni kuwa yale waliyofanya na wakajikurubisha kwacho kwa viabudiwa vyao, basi huko ni kujikurubisha kutupu kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, na walichokifanya kuwa ni cha Mwenyezi Mungu kulingana na madai yao, hicho hakimfikii. Kwa sababu ni shirki, bali ni fungu la washirika na wenza hao. Kwa sababu mwenyezi Mungu hakihitaji, na hakubali matendo ambayo alishirikishwa pamoja naye chochote katika viumbe vyake.