Al-Maaida
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ ٱلْبَحْرِ وَطَعَامُهُۥ مَتَـٰعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ ٱلْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِىٓ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ 96
{96} Na pindi mawindo yalipojumuisha mawindo ya barani na ya baharini, Yeye Mtukufu akayaondoa mawindo ya baharini akisema; “Mmehalalishiwa mawindo ya baharini na kuyala.” Yaani, mmehalalishiwa katika hali ya Ihram yenu "mawindo ya baharini" ambayo ni walio hai miongoni mwa wanyama wake, "na chakula chake" nao ni walio maiti miongoni mwa mwake. Basi hilo likaashiria uhalali wa nyamafu wa baharini. "Kwa faida yenu na kwa wasafiri;" yaani, faida katika kuruhusiwa kwake ni kwa ajili ya manufaa yenu na manufaa ya wale walioandamana nanyi, wanaokwenda pamoja nanyi. "Na mmeharimishiwa mawindo barani maadamu mko katika Ihram;" na inachukuliwa kutoka kwa neno ‘windo’ kwamba ni lazima awe wa mwituni. Kwa sababu yule anayefugwa na binadamu si windo, naye analiwa. Kwa maana asiyeliwa, hawindwi wala haitwi windo. "Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mtakusanywa kwake;" yaani Mcheni Yeye kwa kuyatenda Aliyoyaamrisha na kuyaacha Aliyoyakataza, na tafuteni msaada juu ya kumcha kwa kujua kwamba nyinyi kwa hakika mtakusanywa Kwake, na Atawalipa. Je, mlimfanyia uchamungu wake, ili awalipe thawabu nyingi, au hamkuitekeleza ili awaadhibu?