Al-Maaida
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا۟ ٱلتَّوْرَىٰةَ وَٱلْإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا۟ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَآءَ مَا يَعْمَلُونَ 66
{66} "Na lau kuwa wangeliisimamisha Taurati na Injili na yote waliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wao Mlezi." Yaani, wangetekeleza maamrisho yake [na makatazo yake] kama Mwenyezi Mungu alivyowaamrisha na akawahimiza. Na katika kuisimamisha ni kuyaamini yale inayoyalingania ya kumwamini Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake – na katika Qur-ani. Na lau wangeyasimamisha neema hii kubwa ambayo aliwateremshia Mola wao Mlezi. Yaani, kwa ajili yao na ajili ya kuwatunza, "basi hapana shaka wangelikula vya juu yao na vya chini ya miguu yao." Yaani, Mwenyezi Mungu angeliwaruzuku kwa wingi, na ingeliwanyeshea mbingu, na ingeliwaoteshea ardhi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Na lau kuwa watu wa miji wangeliamini na wakamcha Mungu, kwa yakini tungeliwafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi." "Miongoni mwao;" yaani, katika Watu wa Kitabu, "wapo kaumu walio sawa." Yaani, wafanyao kazi na Taurati na Injili kwa njia isiyo na nguvu wala ya ukakamavu. "Lakini wengi wao wanayoyafanya ni mabaya mno;" yaani, wafanyao mabaya miongoni mwao ndio wengi,. Ama wale wanaofanya kazi miongoni mwao ni wachache tu.