سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
سورت 5

Al-Maaida

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 13

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَـٰقَهُمْ لَعَنَّـٰهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَـٰسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ ٱلْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ ۙ وَنَسُوا۟ حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا۟ بِهِۦ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَآئِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۖ فَٱعْفُ عَنْهُمْ وَٱصْفَحْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ 13

{13} Ni kana kwamba ilisemwa: 'Laiti pia tungejua walichofanya! Walifanya nini? Ne Je, walitimiza kile walichomuahadi Mwenyezi Mungu au walikivunja?' Basi akaeleza kuwa walilivunja hilo, kwa hivyo akasema: "Basi kwa sababu ya kuvunja kwao agano lao," yaani, kwa sababu yake tuliwaadhibu kwa adhabu kadhaa. Ya kwanza ni kwamba, Sisi "tuliwalaani." Yaani tuliwafukuza na kuwaweka mbali na rehema yetu, kwa vile walivyojifungia wenyewe milango ya rehema, na hawakuitimiza ahadi ambayo ilichukuliwa kwao, ambayo ndiyo sababu yake kubwa zaidi. Ya pili ni kauli yake, "Na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu." Yaani, nzito ambazo mawaidha hayaifanyi kitu, wala Aya na maonyo haziinufaishi kitu. Kwa hivyo kushawishiwa hakuwatii moyo, wala kukemewa hakuwatii hofu. Na hii ni katika adhabu kubwa zaidi kwa mja, kwamba moyo wake uwe na sifa hii ambayo haufaidiki na uwongofu na heri isipokuwa shari. Ya tatu ni kwamba wanabadilisha maneno baada ya kuwekwa kwake. Yaani, walipewa majaribio ya kughairi na kubadilisha. Basi wanayapa maneno ambayo Mwenyezi Mungu aliyakusudia maana isiyokuwa ile aliyokusudia Mwenyezi Mungu wala Mtume wake. Ya nne ni kwamba, “walisahau sehemu katika yale waliyokumbushwa kwayo.” Walikumbushwa kwa Taurati na kwa yale Mwenyezi Mungu alimteremshia Musa, lakini wakasahau sehemu katika hayo. Na hili linajumuisha kusahau elimu yake, na kwamba waliisahau na ikawapotea, na hayakupatikana mengi katika yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwasahaulisha ili iwe ni adhabu itokayo kwake juu yao. Na linajumuisha kusahau kuyafanyia kazi ambalo kuacha. Kwa hivyo, hawakuwezeshwa kufanya yale waliyoamrishwa. Na hili linatumika kama hoja dhidi ya Watu wa Kitabu juu ya kukanusha kwao baadhi ya yale yaliyotajwa katika kitabu chao au yaliyotokea katika zama zao kuwa ni katika yale waliyoyasahau. Ya Tano ni hiyana inayoendelea ambayo “huachi kutambua hiyana kutoka kwao.” Yaani, kumfanyia Mwenyezi Mungu hiyana na waja wake Waumini. Na Miongoni mwa hiyana kubwa zaidi kutoka kwao ni kumficha haki yule ambaye anawanasihi na ana dhana nzuri juu yao, na kuendelea kwao kubaki katika ukafiri wao; basi hii ni hiyana kubwa. Na sifa hizi mbaya zinapatikana kwa kila mwenye kusifika kwa sifa zao. Basi kila ambaye hakufanya kile ambacho Mwenyezi Mungu alimuamrisha na akakubali kujukumika kufanya hivyo, basi anakuwa na fungu katika laana hii, na ugumu wa moyo, na kujaribiwa na jambo la kupotosha maneno. Na kwamba hataweza kufanya lililo sahihi, na atasahau fungu katika yale aliyokumbushwa kwayo, na kwamba ni lazima atapewa jaribio la kufanya uhaini. Tunamwomba Mwenyezi Mungu salama. Na Mwenyezi Mungu aliyaita yale waliyokumbushwa kwayo kuwa ni bahati. Kwa sababu hiyo ndiyo bahati kubwa zaidi, na kisichokuwa hiyo, hizo ni bahati tu za kidunia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale waliokuwa wanataka maisha ya duniani: Laiti tungelikuwa tunayo kama aliyopewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa." Na akasema kuhusu bahati yenye manufaa, "Lakini hawapewi wema huu isipokuwa wanaosubiri, wala hawapewi isipokuwa wenye bahati kubwa." Na kauli yake, isipokuwa wachache miongoni mwao, yaani, hao walitimiza yale waliyomuahidi Mwenyezi Mungu, basi akawawezesha na akawaongoa kwenye njia iliyonyooka, "Basi wasamehe na uwaache." Yaani usiwachukulie ubaya kwa yale wanayofanya miongoni mwa udhia ambao inatakiwa wasamehewe, na waache kwani hilo ni katika wema. "Na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema." Na wema ni kwamba umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa humuoni, basi Yeye kwa hakika anakuona. Na kuhusiana na viumbe, ni kuwapa manufaa ya kidini na ya kidunia.