Az-Zukhruf
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَـٰهُ مَثَلًا لِّبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ 59
{59} Kumpendelea Isa [amani iwe juu yake] na uhakika wa kwamba yeye ni katika walio karibu zaidi na Mola wake Mlezi sio jambo linaloonyesha tofauti iliyo baina yake na vyote hivyo katika mahali hapa. Bali ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuwa yeye (Isa) ila ni Mtumwa tuliyemneemesha" kwa unabii, na hekima, elimu, na matendo mema, "tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili" ili wapate kujua kupitia kwake uwezo wa Mwenyeezi Mungu Mtukufu katika kumuumba kwake bila ya baba. Na ama kauli yake Mtukufu: "Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu," jibu lake ni kwa njia tatu: Moja yake ni kwamba kauli yake: "Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu," hapa "hao mnaowaabudu" ni nomino inayoweza kutumika kwa vitu visivyokuwa na akili, ambavyo Masihi na wengineo hawajumuishi ndani yake. Ya pili ni kwamba maneno haya wanaambiwa washirikina walioko Makka na wale walioko pembezoni mwake. Nao walikuwa wakiabudu masanamu na miungu tu, na wala hawakuwa wakimuabudu Masihi. Ya tatu ni kwamba Mwenyezi Mungu alisema baada ya aya hii: "Ama hakika wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa mbali na hayo." Na hakuna shaka yoyote kwamba Isa na manabii wengineo katika vipenzi wa Mwenyezi Mungu wamejumuishwa katika aya hii.