سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
سورت 4

An-Nisaa

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 66

وَلَوْ أَنَّا كَتَبْنَا عَلَيْهِمْ أَنِ ٱقْتُلُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ أَوِ ٱخْرُجُوا۟ مِن دِيَـٰرِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٌ مِّنْهُمْ ۖ وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا۟ مَا يُوعَظُونَ بِهِۦ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا 66

{66} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba lau angewaandikia waja wake maamrisho mazito juu ya nafsi, kama vile kuiua nafsi na kuondoka katika maboma, basi hawangelifanya hiyvo isipokuwa wachache tu kati yao na walio nadra. Basi wamhimidi Mola wao Mlezi na wamshukuru kwa kuwasahilishia aliyowaamrisha miongoni mwa maamrisho ambayo ni mepesi kwa kila mtu, na wala si magumu kuyafanya. Na katika hili kuna ishara kwamba mja anafaa pia kuzingatia kinyume cha yale aliyomo ya machukizo; ili ibada ziwe nyepesi kwake, na azidishe kumhimidi na kumshukuru Mola wake Mlezi. Kisha akajulisha kwamba ikiwa wao “wangelifanya yale wanayowaidhiwa kwayo." Yani walichoamrishwa katika kila wakati kwa mujibu wake, na wakafanya juhudi, na wakajitolea nafsi zao katika kukifanya na kukikamilisha, na nafsi zao zisitamani yale ambayo haziyafikii, na wala hawayakanushi. Na hili ndilo jambo analopaswa mja, kwamba atazame hali anayotakiwa kuifanya, na aikamilishe kidogo kidogo, mpaka afikie kile alichoandikiwa katika elimu na matendo katika mambo ya dini na dunia. Na hili ni kinyume na yule ambaye nafsi yake inatamani kitu ambacho hawezi kukipata na bado hajaamrishwa kukifanya, basi yeye hakaribii kulifikia kwa sababu ya kutawanyika kwa azimio lake, na kupatwa na uvivu, na kutokuwa na nishati. Kisha akafungamanisha yale yatakayowapata kwa sababu ya kufanya yale wanayowaidhiwa kwayo, na ni mambo manne: La kwanza yake: Ubora katika kauli yake, "ingelikuwa bora kwao" Yani wangekuwa miongoni mwa walio bora, wanaosifika kwa sifa zao kama vile matendo mema ambayo waliamrishwa. Yani hilo lingewaondolea sifa ya waovu. Kwa sababu, kuthibiti kwa kitu kunalazimu kutokuwepo kinyume chake. La pili: Kupata kuimarishwa na kuwa imara na zaidi yake. Kwani Mwenyezi Mungu huwaimarisha wale walioamini kwa sababu ya yale waliyoyafanya ya kuamini, ambayo ni kufanya waliyowaidhiwa kwayo. Kwa hivyo, anawaimarisha katika maisha ya dunia fitina inapotokea katika maamrisho, na makatazo, na misiba. Basi wanapata uthabiti ambao wanawezeshwa kwao kufanya maamrisho na kuacha makemeo ambayo nafsi inataka kuyafanya kwa lazima. Na wakati inapotokea misiba ambayo mja anaichukia. Kwa hivyo, anawezeshwa kuimarishwa kwa kuwezeshwa kuwa na subira au kuridhia au kushukuru. Basi anateremkiwa na msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili kufanya hivyo, na wanapata uthabiti katika dini wakati wa kufa na katika kaburi. Na pia, mja anayefanya yale aliyoamrishwa, haachi kuendelea kujizoesha kutekeleza maamrisho ya kisheria mpaka ayazoee, na awe na shauku nayo, na juu ya kuyatekeleza. Kwa hivyo, hilo linakuwa msaada kwake kuwa imara juu ya utiifu.