An-Nisaa
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
وَٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۗ وَمَن يَكُنِ ٱلشَّيْطَـٰنُ لَهُۥ قَرِينًا فَسَآءَ قَرِينًا 38
{38} Kisha akajulisha juu ya matumizi yatokanayo na kujionyesha, kutaka sifa, na kutokuwa na imani naye, akasema, “Na ambao hutoa mali zao ili kujionyesha kwa watu.” Yani ili wawaone, na kuwasifu, na kuwatukuza. “wala hawamwamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho.” Yani kutoa kwao matumizi hakutokani na kumkusudia na kumuamini Mwenyezi Mungu peke yake na kutaraji thawabu zake. Yani hizi ni katika hatua za Shetani na matendo yake ambayo anawalingania kundi lake ili wawe miongoni mwa wenza wa Moto wenye mwako mkali, na kulitoka kwao kwa sababu ya yeye kuwa mwenza wao na kuwahimiza kufanya hivyo. Ndiyo maana akasema, “Na yule ambaye Shetani amekuwa ndiye mwenza wake, basi ana mwenza mbaya mno.” Yani mwenza mbaya zaidi na sahibu ni yule anayetaka kumwangamiza yule anayemfanya kuwa mwenza, na akafanya juhudi kubwa sana katika hilo. Na kama vile mwenye kufanyia ubahili yale ambayo Mwenyezi Mungu alimpa, na akaficha yale aliyomneemesha nayo Mwenyezi Mungu ni muasi, mwenye dhambi, anayemhalifu Mola wake Mlezi, kadhalika anayetoa na kumfanyia ibada asiyekuwa Mwenyezi Mungu, yeye pia ni mkosaji, mwenye kumuasi Mola wake Mlezi, na anastahili adhabu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu aliamrisha utiifu kwake tu, na kufuata amri yake kwa njia ya kumfanyia Yeye tu. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Nao hawakuamrishwa isipokuwa kwamba wamwabudu Mwenyezi Mungu kwa ikhlas (nayo ni kumfanyia Yeye peke yake tu) katika Dini.” Na kwa sababu hii, matendo yanayokubalika, ni yale ambayo mwenyewe anastahili sifa na thawabu. Ndiyo maana Mola Mtukufu akamhimiza juu yake kwa kauli yake: