An-Nisaa
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَكُم بُرْهَـٰنٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا 174
{174} Yeye Mtukufu anawabainishia neema yake watu wote kwa sababu ya kile alichowafikishia miongoni mwa ushahidi wa uhakika na nuru iliyo wazi, ili kusimamisha hoja juu yao na kuwabainishia njia ya uwongofu. Akasema, "Enyi watu! Hakika umekwisha wafikia ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, hoja za uhakika juu ya haki, zenye kuibainisha, na kuiweka wazi, na zinabainisha kinyume chake. Na hili linajumuisha ushahidi wa kiakili na wa kimaandiko, na ishara za upeo wa macho na za kisaikolojia, "utawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli." Na katika kauli yake, "Kutoka kwa Mola wenu Mlez,"} kuna kinachoonyesha utukufu wa ushahidi huu na ukubwa wake. Kwa kuwa umetoka kwa Mola wenu Mlezi aliyekulea kwa malezi ya kidini na ya kidunia. Na katika malezi yake kwenu amabyo anasifiwa kwa huo, na kushukuriwa ni kwamba aliwafikishia hoja zilizo wazi ili awaongoze kwazo kwenye Njia iliyonyooka yenye kufikisha katika Mabustani yenye neema. Na akateremsha "kwenu nuru iliyo wazi." Nayo ni Qur-ani hii tukufu, ambayo imejumuisha elimu za watu wa mwanzo na wa mwisho, na habari za kweli, zenye manufaa, na amri ya kila uadilifu, na wema, na heri, na kukataza kila dhuluma na uovu. Basi Watu wako katika giza ikiwa hawajaiangaza kwa nuru zake. Na katika taabu kubwa ikiwa hawatachukua katika heri yake.